Van Vicker akunwa na Maua Sama

Dimba - - Burudani Za Wasanii - NA JESSCA NANGAWE

BAADA ya staa wa Filamu Nigeria, Van Vicker, kuposti kipande cha video ya wimbo wa 'Iokote' wa msanii Maua Sama, mwenyewe ameibuka na kudai ngoma hiyo imemwongezea mashabiki na kupokelewa kwa aina ya utofauti. Ngoma hiyo, ambayo imeendelea kufanya vyema sehemu mbalimbali, imezidi kufanya vizuri mara baada ya juzi msanii huyo kutoa video yake. Akizungumza na DIMBA Jumatano, Maua Sama alisema, video ya ngoma hiyo imechelewa kutoka baada ya kukumbwa na matatizo yaliyosababisha kufikishwa mahakamani yakihusisha wimbo huo. ìNi ngoma ambayo naona imenipeleka kwenye hatua nyingine, mapokezi yake yamekuwa ya kitofauti kuliko ngoma zangu zilizopita, msanii kama Van Vicker kuonekana kuikubali, kwangu ni faraja ya kipekee na inazidi kunipa moyo,î alisema.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.