WAKALI HAWA WAMEREJEA, PATACHIMBIKA

Dimba - - Burudani Za Wasanii -

WACHEZAJI wanne tegemeo katika vikosi vya Yanga, Simba na Azam, ghafla walijikuta mwishoni mwa wiki iliyopita pamoja na juzi Jumatatu wakirejea kwa pamoja kuongeza nguvu kwenye timu zao. Iko hivi. Jumamosi Haruna Niyonzima na Juuko Murshid walionekana kuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichovaana na African Lyon ikiwa ni mara yao ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu, kutokana na sababu mbalimbali. Kwa upande wa Yanga, Thaban Kamusoko pia alifanikiwa kushuka dimbani kwa mara ya kwanza kipindi cha pili cha mchezo uliowakutanisha na Mbao akichukua nafasi ya Deus Kaseke dakika ya 56. Lakini pia Yakub Mohamad wa Azam akionekana katika benchi, Wanalambalamba hao wakionyeshana kazi na Coastal Union, ikiwa ni baada ya Mghana huyo kupona majeraha yake ya muda mrefu yaliyomkumba msimu uliopita.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.