DONOA DONOA

Dimba - - Burudani Za Wasanii - NA MAREGES NYAMAKA

LAURIAN MPALILE

NAHODHA wa timu ya Tanzania Prisons anasema kati ya mchezo ambao unampa wakati mgumu wanapokuwa wamepoteza, ni dhidi ya wapinzani wao kutoka jiji moja, Mbeya City. Mchezo huo maarufu kama ‘Mbeya Derby’ ulipigwa mwishoni mwa wiki iliyopita na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 baada ya sare kutawala misimu ya karibuni.

MOHAMMED HUSSEIN

KIUNGO wa pembeni wa Simba anaamini upinzani wa nafasi msimu huu umeongezeka maradufu kikosini hapo kitendo kinachomfanya kila mmoja kupambana kulishwawishi benchi la ufundi kupata nafasi ya kucheza. Anasema kwamba kwa upande mwingine ni jambo zuri kuwa na kikosi kipana kulingana na michuano wanayoshiriki, huku lengo likiwa ni kusaka matNAHODHA aji.

ABDALLAH SHAIBU ‘NINJA’

BEKI wa kati wa Yanga anaweka wazi kuwa huenda tangu ajiunge na Yanga akitokea Taifa Jang’ombe ya visiwani Zanzibar, mchezo aliocheza kwa akili nyingi sawa na matumizi ya nguvu ulikuwa dhidi ya Simba Septemba 30, mwaka huu. Hadi mchezo huo wa watani wa jadi unamalizika, nyota huyo anayetajwa kama mrithi wa Nadir Haroub ‘Cannavaro’, hakuwa ameonyeshwa kadi ya njano isipokuwa alionywa kwa mane- no na

ELIUD AMBOKILE

STRAIKA wa Mbeya City anasema anawashukuru wachezaji wenzake kucheza kwa ushirikiano, kwani bila wao yeye si kitu chochote katika kutimiza jukumu lake la kuweka mpira kimiani kama ambavyo amekuwa mwiba kwa mabeki. Kinara huyo wa mabao (6) kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, katikati ya wiki iliyopita alitangazwa na Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuwa ndiye mchezaji bora wa mwezi Septemba.

DAVID MWASA

wa timu ya Mbao anasema makosa mawili waliyoyafanya idara ya ulinzi yaliwagharimu na kujikuta wakipoteza mbele ya wenyeji wao, Yanga, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Waranda mbao hao waliendelea kupata wakati mgumu kuvuna pointi tatu wakikosa hata sare dhidi ya Yanga katika uwanja huo tofauti na wanavyokuwa dimba lao la nyumbani, CCM Kirumba.

UHURU SELEMAN

WINGA wa timu ya Biashara United ya Musoma, mkoani Mara, amewataka mashabiki wa kikosi hicho waendelee kuwapa sapoti licha ya kuambulia kichapo mwishoni mwa wiki mchezo wa ligi uliowakutanisha na Mwadui. Hata hivyo, nyota huyo bado ana mlima mrefu kupanda kukisaidia kikosi hicho kutokana na nyota walio wengi kukabiliwa na ugeni wa ligi ambapo wameshinda mechi moja pekee na kukumbana na kichapo mara nne na sare tatu.

YAYHA ZAYD

STRAIKA kinda wa Azam anasema yuko tayari kucheza sambamba na nyota yeyote katika safu hiyo ya ushambuliaji kwani hayo ni majukumu ya kocha wake, Hans van der Pluijm. Zayd amekuwa kwenye ubora mkubwa katika mechi mbili zilizopita akicheza sambamba na Mzimbabwe Donald Ngoma, wakioneshwa uewelano wa kuvutia kwa haraka zaidi.

MBWANA MAKATA

KOCHA wa Alliance ya Mwanza anasema mapambano yanaendelea, pamoja na kukumbana na changamoto kadhaa ikiwamo maamuzi mabovu ya waamuzi tofauti na mitazamo ya makundi mbalimbali kuwa kikosi chao kinacheza soka la shule. Anasema licha ya mapungufu kadhaa hasa katika safu ya ushambuliaji kumalizia mpira kimiani, bado wana nafasi ya kuwashangaza wanaowazodoa lakini pia akiwataka waamuzi wafuate sheria 17 zinazowaongoza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.