JOHN TERRY

ATABAKI KUWA ALAMA YA CHELSEA

Dimba - - Burudani Za Wasanii -

LONDON, ENGLAND B AADA ya kucheza soka la ushindani kwa miaka 23, nahodha wa zamani wa Chelsea, John George Terry, ametangaza rasmi kustaafu na kujielekeza katika mambo mengine.

Terry alitangaza uamuzi huo usiku wa Jumapili kupitia ukurasa wake wa Instagram: “Baada ya miaka 23 ni wakati sahihi mimi kustaafu kucheza soka,” alisema Muingereza huyo.

Beki huyo wa kati mwenye urefu wa futi sita ametundika daluga akiwa na miaka 37, huku klabu yake ya mwisho kukipiga ikiwa ni Aston Villa inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza (Championship).

Katika muda wa miaka 23 ndani ya timu yake ya Taifa ya England, amefanikiwa kucheza jumla ya mechi 78 pekee akiingia nyavuni mara sita.

Upande wa familia ni baba mwenye watoto wawili mapacha, Georgie John na Summer John waliozaliwa Mei 18, 2006 wote wakizaliwa ndani ya ndoa na mkewe Toni. Mkali huyo wa mabao ya vichwa leo pointi tano zinatoka kwake ikichagizwa na alivyolitendea haki soka akiwa na klabu ya Chelsea iliyomsajili mwaka 1995 akitokea Academy ya West Ham United ya jijini London.

NAHODHA WA KIHISTORIA

Mei 19, 2017 aliteuliwa kuwa nahodha wa kwanza kuiongoza Chelsea na kuwatungua Manchester United bao 1-0 mchezo wa kwanza wa Kombe la FA ndani ya Uwanja wa Wembley, bao likifungwa na Didier Drogba. Lakini pia akiwa mchezaji w a kwanza kufunga b a o alilofungwa kwa kichwa dimba hilo akiwa na timu yake ya Taifa ya England katika sare ya 1-1 dhidi ya Brazil. Kama hiyo haitoshi, anabaki kuwa nahodha wa aina yake kuwaongoza wachezaji wenzake

MATAJI 17, UEFA NDANI

Miaka 22 aliyodumu na The Blues amefanikiwa kutwaa mataji 17, matano, Premier League: 2004/05, 2005/06, 2009/10, 2014/15, 2016/17 ni kama ilivyo upande wa Kombe la FA: 1999/ 2000, 2006/07, 2008/09, 2009/10, 2011/12.

Idadi kama hiyo ya mataji pia alinyanyua Kombe la Ligi: 2004/05, 2006/07, 2014/15.

Ngao ya Jamii: 2005, 2009. UEFA: 2011/12 pamoja na UEFA Europa: 2012/13.

BEKI BORA ULAYA MARA TATU

Umahiri wake miaka ya 2005, 2006 na 2009 uliwashawishi mabosi wa Chama cha Soka barani Ulaya (UEFA) kumtangaza beki bora kwa nyakati hizo tofauti.

SHABIKI WA MANCHESTER UNITED

Terry akiwa mdogo alikuwa shabiki mkubwa wa Manchester United, alikiri hilo mwaka 2005 alipokuwa akifanya mahojiano na moja ya kituo cha runinga jijini London. Achepuka na shemeji yake Januari 2010 alikuwa katika wakati mgumu baada ya kuhusishwa na kashfa ya kuchepuka katika ndoa yake akidaiwa kutoka kimapenzi na mrembo, Vanessa Perroncel, ambaye alikuwa mke wa zamani wa mchezaji mwenzake hapo Chelsea, Wayne Bridge.

Uhusiano wa wawili hao unadaiwa ulidumu kwa miaka minne kabla ya mambo kuwekwa hadharani, kitendo ambacho kilimfanya nyota huyo ndoa yake kuyumba.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.