Kumbe Mzungu wa A. Lyon ni mkalimani

Dimba - - Burudani Za Wasanii - NA ABDULAH MKEYENGE

UKIACHANA na jukumu la kuwa nahodha mkuu katika mchezo wa Simba dhidi ya A. Lyon, Uwanja Taifa, jijini Dar es Salaam, mshambuliaji wa Lyon, Victor da Costa, ana kazi nyingine ndani ya kikosi hicho.

Costa ambaye raia wa Ufaransa amekuwa na kazi ya ukalimani ndani ya kikosi hicho akimsaidia kocha wake, Soccoia Lionel, akihojiwa na waandishi wa habari Tanzania, kutokana na Lionel kutojua lugha ya Kiingereza na Kiswahili.

Muda mrefu katika mahojiano ya waandishi na Lionel, Costa alikuwa akimsaidia kusikiliza maswali ya waandishi na kumwambia Lionel ambaye naye alijibu maswali hayo kupitia kwa Costa na Costa aliwajibu waandishi kwa Kiingereza.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.