Karia ashtushwa kujiuzulu bosi TFF

Dimba - - Burudani Za Wasanii - NA CLARA ALPHONCE

RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia, ameshtushwa na uamuzi wa wa kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo, Revocatus Kuuli.

Hivi karibuni Kuuli aliiandikia barua TFF na kutangaza kuachia ngazi nafasi yake kwa madai ya kukerwa na kitendo cha Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau, kuingilia majukumu ya Kamati yake.

Karia alisema mpaka sasa hajui nini kimetokea na kumfanya Wakili huyo msomi kuchukua maamuzi maagumu wakati tayari alikuwa katika harakati za kulimaliza tatizo hilo.

ìNilisikia taarifa za malumbano kati ya Kidau na Kuuli nikiwa nje ya nchi, niliwasiliana na Katibu wangu ili kujua kama kuna tatizo, naye aliniambia kuwa atanipa maelezo, ila hakukuwa na tatizo lolote.

ìNikashangaa kusikia Mwenyekiti Kuuli anazungumza na vyombo vya habari kuhusu suala hilo, niliporudi niliwaita wote na kuomba maelezo zaidi ya suala hilo, siku moja baadaye Kuuli ananiletea barua ya kujiuzuu wakati hajaleta maelezo yoyote,î alisema Karia.

Hata hivyo, Rais huyo wa TFF, alisisitiza kuwa pamoja na kuandika barua ya kujiuzulu, bado ataomba maelezo yake juu ya hilo lililotokea, ili jamii iweze kujua nini kinaendelea kati yao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.