Lwandamina aifuata Simba CAF

Dimba - - Burudani Za Wasanii - NA JESSCA NANGAWE

WAKATI msimu mpya wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ikipangwa kuanza Desemba mwaka huu, mabingwa wa Ligi Kuu nchini Zambia, Zesco, ambao wananolewa na kocha wa zamani wa Yanga, George Lwandamina, huenda wakakutana na mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba.

Kwanini wanaweza kukutana na Simba. Jibu ni rahisi tu. Waandaaji wa michuano hiyo, Shirikisho la Soka Barani (CAF) wamebakiza mwezi mmoja tu kabla ya kuanika ratiba ya makundi kwa timu shiriki na inaweza kutokea Simba na Zesco wakatupwa kundi moja.

Jumapili iliyopita Zesco walitangazwa kuwa mabingwa wa nchi hiyo na hivyo kukata tiketi ya kucheza michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.Ikitokea hivyo, itakuwa ni kazi mpya kwa Lwandamina kufanya kila awezalo ili kuifunga Simba, kwani ikumbukwe katika kipindi chote alichokuwa Tanzania akiinoa Yanga alishindwa kufanya hivyo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.