JUVE HAWANA MPANGO NA POGBA

Dimba - - Burudani Za Wasanii - TURIN, Italia

KWA mujibu wa Mkurugenzi wa Ufundi wa Juventus, Fabio Paratici, hawana mpango wa kumrejesha kiungo Mfaransa, Paul Pogba, kama ambavyo wanahusishwa kusaka saini yake.

Pogba aliyehudumu viunga vya Turuni kuanzia mwaka 2012 kabla ya kurejea Old Trafford 2016 kwa kitita cha pauni milioni 89, amekuwa akihusishwa kuondoka klabuni hapo ikichagizwa na mahusiano mabovu kati yake na Jose Mourinho.

Lakini upande wa Juventus, wamebainisha hawana mpango kabisa wa kumsajili mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwenye umri wa miaka 25.

"Tunampenda sana, tunahitaji kuona akifanya vizuri zaidi, lakini si chaguo letu katika usajili wala hatulifikirii hilo, huo mjadala ufungwe, tunaye Cristiano Ronaldo,” alisema Paratici.

Juventus wanaamini katika usajili wa Cristiano Ronaldo ‘Cr 7’ mwenye umri wa miaka 33 waliomchomoa Real Madrid kwa kitita cha pauni milioni 105, ni msaada mkubwa kwao.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.