HIYO DOZI YA UNAI NI NOMA

Dimba - - Burudani Za Wasanii -

U NAAMBIWA hayo mazoezi ya kocha wa Arsenal, Unai Emery, kama mchezaji mvivu baki nyumbani kwako ucheze na familia yako tu.

Wachezaji wa Arsenal walibainisha kuwa linapokuja suala la mazoezi, kocha huyo huwa mkali na mwenye kufuatilia kila hatua huku akiwa na taarifa ya kila mchezaji kwa kinachoendelea.

“Ana mazoezi magumu, hapendi wachezaji wavivu kabisa, kila kinachoendelea hufuatilia kwa ukaribu ili kujua, tunajivunia kuwa naye,” alisema mchezaji wa zamani wa Arsenal ambaye hivi sasa ni kocha wa kikosi cha vijana, Per Metersacker.

Mpaka sasa Arsenal imefanikiwa kushinda michezo tisa mfululizo katika michuano yote na kutoa matumaini makubwa kwa mashabiki wa klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.