Maumivu -8

Dimba - - Burudani Za Wasanii - ITAENDELEA... Je, nini kitatokea? Usikose wiki ijayo. Karibu kwa maoni yako 0718-400146.

ILIPOISHIA... Kile ki – memo hakikuwa na maneno mengi. Kiliandikwa hivi: Karibu sana Tanga. Kama hutajali, ningependa niwe mwenyeji wako. Namba zangu ni 0841 17074512. Tunu. Moyo wake ukapasuka, akageuza macho yake na kumtazama yule msichana. Akampokea kwa tabasamu pana. Tabasamu mwanana. Tunu alikuwa tunu kweli, tabasamu lake likamwongezea uzuri wake. SASA ENDELEA... TUNU toto la Kitanga! Bruno hoi! *** Kuachana na Emma ndiyo wazo alilolala nalo Vanessa, pia wazo hilo hilo aliamka nalo kichwani mwake. Hakutamani kabisa kuwa na Emma, mwanamume mkorofi, anayempiga kila siku, anayemnyanyasa, anayemuonea! Hakuwa na thamani tena katika maisha yake. Aliapa kumuacha! “Lazima niachane naye, lazima,” akatamka kwa sauti ya chini akionekana kuwa na uchovu mwingi wa usingizi.

Mara moja akachukua simu yake iliyokuwa mezani, kisha akabonyeza jina la Bruno haraka. Alitamani sana kuzungumza naye, akiamini angekuwa msaada mkubwa wa mawazo tele aliyokuwa nayo kichwani mwake. Muda si mrefu, sauti ya upande wa pili ilisikika; alikuwa ni Bruno akiongea kwa sauti ya taratibu. “...umeamkaje Bruno?” “Salama, vipi wewe?” “Sijambo kabisa.”

“Yeah, ndiyo nimeamka muda huu, nikafikiria naweza kufanya kitu gani kama cha kwanza kwa leo, nikaona bora nikupigie wewe, nikusalimie, hili ndilo jambo nililoamua kulifanya la kwanza kwa leo.”

“Nashukuru sana Vanessa, naweza kukuuliza jambo?” “Yeah!” “Kwanini umenichagua mimi kuwa wa kwanza kuanza ratiba zako za leo?”

“Tupo karibu Bruno, sisi ni marafiki wakubwa sasa, marafiki wa karibu sana Bruno.” “Hakuna kingine?” “Kipi? Au wewe unacho?” “Sidhani, lakini kama ndivyo, nashukuru sana maana naona nitakuwa nina nafasi kubwa sana kwako.”

“Ni kweli kabisa, ipo nafasi kubwa sana moyoni mwangu kwa ajili yako.” “Ahsante sana.” “Basi nikutakie asubuhi njema, baadaye nitakuja kukuangalia.”

“Nashukuru sana, ahsante sana Vanessa, nawe nakutakia kila la kheri katika siku yako ya leo. Mungu awe taa yako!”

“Nashukuru kwa baraka zako.” “Ok!” Wakakata simu zao. Vanessa akavuta pumzi ndefu sana kisha akazishusha taratibu kabisa, akatabasamu. Taratibu akamvuta Bruno kichwani mwake, akamwangalia akiwa amesimama mbele yake; naam! Alikuwa mwanamume thabiti kwake. Anayejiheshimu, mwenye mapenzi ya dhati, mwenye upendo wa ndani, mvumilivu na kila sifa njema, akammiminia Bruno.

Akatabasamu tena.

“Yeah! Yule ndiyo mwanaume, mwenye kauli njema na kujua kubembeleza, najua nikimsogeza kwangu, nitakuwa na amani. Ninazo fedha, lakini sina amani. Nahitaji amani ya moyo wangu. Naamini ipo kwake, nitajitahidi sana niipate,” anawaza Vanessa akiwa amesimama na kanga moja kifuani.

Anatoka nje na kusaidiana usafi na msichana wake wa kazi. *** Alishasahau kabisa kwamba mkononi mwake ameshika glasi yenye kinywaji, aliulegeza mkono wake, macho yake yakiwa bado yanamwangalia yule msichana aliyemtumia kikaratasi chenye ujumbe. Akarudia kusoma kwa mara ya pili, halafu akarudisha macho yake tena kwa yule msichana.

Akakaribishwa na tabasamu mwanana kabisa. Naye akajibu. Wakatazamana wakitabasamu. Punde kile kinywaji ndani ya glasi, kikaanza kumwagika!

“Oyaaa vipi mkubwa, unanichafua!” Alikuwa ni rafiki yake aliyekaa meza ya jirani.

“Oh! I’m sorry kaka, sikukuona.”

“Usijali, lakini kuwa mwangalifu.” “Poa.” Kazi ikaendelea kuwa ile ile, lakini muda kidogo, akiwa kama amegutuka hivi, akaiandika ile namba ya simu kwenye simu yake, kisha akaihifadhi. Alichokifanya ni kwenda kwenye sehemu ya kuandika ujumbe mfupi, kisha akaandika ujumbe na kutuma kwenda katika ile namba.

Ulisomeka hivi; “Ahsante Tunu, nimefurahishwa sana na ukarimu wako.”

“Nami pia, nimevutiwa sana na wewe. Naomba usitafsiri vibaya, nimevutiwa na wewe....” Tunu akamtumia.

“Ahsante kwa hilo, unaishi maeneo gani kwa hapa Tanga?” “Mabawa.” “Ni mbali sana kutoka hapa?” “Hapana...sijui mwenzangu unaitwa nani?” “Bruno.” “Najua ni mgeni, unatokea wapi?”

“Kiukweli hapa Tanga siyo mgeni sana, kwani ni mara ya sita sasa nakuja hapa.” “Ni mfanyabiashara?” “Hapana ni mfanyakazi wa mfanyabiashara!”

“Sawa, karibu sana Bruno, kama nilivyokuambia, nimependa sana kampani yako... kama hutajali ningependa ulale kwangu kwa kipindi chote utakachokuwa hapa.” “Nilale kwako?” “Ndiyo...nina nyumba kubwa Bruno, hata chumba cha wageni pia ninacho, nadhani kitakufaa.”

“Nitashukuru....acha niongee kwanza na wenzangu, halafu nitakujulisha.” “Sawa.” Bia zikaendelea kunyweka, huku Bruno akichati na Tunu, baadaye Tunu akahamia kwenye meza ya akina Bruno kabisa, wakaendelea kukata maji kama kawaida. Muda wa kuondoka, Bruno akaomba kwenda kulala na Tunu. Hakuna aliyemzuia, kila mtu alikuwa amelewa.

“Sasa Tunu, twende zetu,” Bruno akamwambia Tunu ambaye aliitikia kwa kutingisha kichwa huku akijitahidi kuamka kwa kuyumba kidogo.

Wakashikana mikono na kwenda kwenye taxi. Wakaingia na kuketi wote siti ya nyuma. Mabusu ukawa ndiyo wimbo mzuri kwao kwa usiku huo. *** Waliingia kwenye chumba kimoja kizuri chenye mpangilio wa kuridhisha. Kilikuwa chumba kimoja chenye kila kitu ndani, choo na bafu vilikuwa ndani. Ile kuingia tu, Tunu akavua nguo zote harakaharaka, akamsogelea Bruno na kuanza kumvua.

“Vipi?” Bruno akauliza, pombe ikianza kumtoka. “Nataka twende bafuni.” “Si ulisema kuna chumba changu?”

“Acha ujinga, utaniaibisha mwanaume. Hebu vua nguo twende bafuni, tuoge tuje tulale.”

Bruno akawa mpole, akapelekwa bafuni na kuogeshwa kwa maji ya karafuu. Starehe zote alizisikia. Neno moja tu, lilimponyoka; “Hivi Tunu hujaolewa?”

“Bado, kwani unataka kunioa?”

“Nitakuwa muongo, nilitaka tu kujua.” “Sijaolewa.” “Huna bwana anayekuja hapa?” Swali hili aliuliza akionekana kuwa na mashaka kidogo.

“Sina, kwanini una mashaka sana? Unadhani mimi ni mwanamke mpumbavu wa kiwango gani nikulete kwenye nyumba ambayo ina mmiliki wake? Bruno jiamini,” Tunu akasema, akimbusu midomoni mwake, kisha akamsukuma kitandani.

Akazima taa.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.