Singida United: Hata Simba na Yanga zina njaa

Dimba - - News - NA SALMA MPELI

UONGOZI wa Singida United umesema kwamba, kuondoka kwa wachezaji wao kutokana na suala la madai ya mishahara na ada ya kusaini mikataba, ni jambo la kawaida, kwani linaweza kutokea kwenye timu yoyote hata Simba na Yanga.

Hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka wimbi kubwa la wachezaji waliokuwa wanaitumikia timu hiyo kuondoka, huku sababu kuu ikitajwa ni madai ya fedha za mishahara na ada za kusaini ambayo hawajamaliziwa.

Akizungumza na DIMBA, Mkurugenzi wa Singida ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Klabu hiyo, Festo Sanga, alisema kutokana na mwenendo wa Ligi kwa sasa na hali ngumu ya kimaisha, kudaiwa si dhambi.

UTETEZI

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.