Simba yajibu mapigo kwa Yanga

Dimba - - News - NA SALMA MPELI

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, wamekuwa moto wa kuotea mbali kwa sasa baada ya kuwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga katika michezo 10 waliyocheza hadi sasa.

Simba wameonekana kama wamekuja kivingine, kwani katika michezo miwili iliyopita, wamefanikiwa kufunga jumla ya mabao 10, huku wao wakiruhusu kufungwa bao moja peke yake.

Kutokana na kasi hiyo kubwa ya ufungaji wa mabao mengi kwa Simba, ni kama imejibu mapigo kwa wapinzani wao, Yanga, ambao wakati Ligi inaanza msimu huu, walikuwa wanaongoza kupachika mabao mengi.

Mpaka sasa Simba wamefanikiwa kufunga jumla ya mabao 21 katika michezo 10 waliyocheza, huku Yanga wakiwa wamefunga mabao 15 katika michezo nane kabla ya mchezo wao wa jana dhidi ya Lipuli FC.

MPAMBANO

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.