Straika Simba ajipigia debe

Dimba - - News - NA TIMA SIKILO

STRAIKA Mtanzania, Elias Maguli, ambaye alishawahi kuichezea Simba, amesema yupo huru kusajili timu yoyote ambayo itamhitaji kuelekea dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Novemba 15, mwaka huu.

Maguli, ambaye pia amewahi kuzichezea Dhofar SC ya Oman, Ruvu Shooting ya Pwani, Stand United ya Shinyanga pamoja na timu ya Taifa ya Taifa Stars, kwa sasa yupo nchini.

Maguli juzi alionekana katika Uwanja wa Taifa kuishuhudia African Lyon dhidi ya Biashara, ambapo ameliambia DIMBA Jumatano kwamba, timu itakayochangamkia fursa itampata kilaini.

Maguli alisema amemaliza mkataba na timu yake ya AS Kigali ya nchini Rwanda, ambayo kwa sasa inanolewa na Kocha Masoud Djuma, na kwamba yupo huru kusajili timu nyingine.

USAJILI

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.