ZAHERA AFUNGUKA KUSUSA KWA AJIB

Dimba - - Mbele - NA SALMA MPELI

STARIKA wa Yanga, Ibrahim Ajib, jana alikosa mechi yake ya pili mfululizo wakati timu yake ilipowakabili Lipuli FC, baada ya awali kukosa mechi dhidi ya KMC, kutokana maumivu ya mgongo, lakini hata hivyo, jambo hilo limeleta mjadala.

Taarifa ambazo zimezagaa mitandaoni zinadai kuwa, Ajib amekerwa na maneno ya kocha wake Mkuu, Mwinyi Zahera, zinazomlaumu mara kwa mara kwamba amekuwa mvivu na hajitumi kikosini.

Hata hivyo, Zahera amewajia juu wote wanaotoa maneno hayo, akidai wanamsingizia mchezaji wake, kwani ana matatizo ya mgongo.

ìMimi ninachojua ni kwamba Ajib anaumwa, sasa hayo mambo mengine siyajui, hawezi kuweka mgomo wa namna hiyo.

ìKama kweli ni ujanjaujanja itajulikana tu lakini ninachofahamu ni kwamba Ajib anaumwa na hata daktari amelithibitisha hilo,î alisema.

Ajib alionekana kuja kwa kasi msimu huu baada ya kufunga mabao matatu kutokana na mechi sita alizocheza, huku akitoa pasi za mwisho za mabao saba.

Lakini Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, alieleza kutoridhishwa na kiwango cha mchezaji huyo, licha ya kufunga na kusaidia kupatikana kwa mabao mengi, huku akimtaka kujituma zaidi.

Kutokana na kauli hizo za kocha, ndipo yakatokea maneno kwamba Ajib ameamua kususa, lakini Zahera mwenyewe kajitokeza na kudai mchezaji wake ni mgonjwa na wala hana tatizo lingine.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.