Messi amponza kocha mpya Real Madrid

Dimba - - Mbele -

SAHAU kuhusu kipigo cha bao 1-0 walichokipata Tottenham kutoka kwa Manchester City katika mchezo uliopigwa usiku wa kuamkia jana kwenye Uwanja wa Wembley.

Mashabiki wa Tottenham wamefurahishwa na kitendo cha kiungo wa kikosi hicho, Dele Alli, kusaini mkataba mpya wa miaka sita ambao utamweka ndani ya timu hiyo mpaka mwaka 2024, huku akipokea mshahara kiasi cha pauni 90,000 kwa wiki.

Tangu kuanza kwa msimu huu Tottenham inayonolewa na Mauricio Pochettino, imefanikiwa kuwaongezea mikataba wachezaji tegemeo ndani ya timu hiyo.

Harry Kane, Son Heung-Min na wengine walisaini mikataba ya muda mrefu ya kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake London, nchini England.

“Nafurahi kusaini mkataba mpya tena hapa, kila muda nilioutumia hapa niliufurahia, tutakuwa pamoja mpaka 2024,” alisema Dele.

Tottenham ilimsajili kiungo huyo raia wa England mwaka 2015 katika kikosi cha MK Dons, hadi sasa Dele amefunga mabao 48 kwenye michezo 153 michuano yote.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.