Mkakati huu wa Simba hakuna atakayepona

Dimba - - News - CLARA ALPHONCE NA SAADA SALIM

KAMA ulikuwa unafikiri Simba wamebweteka na ushindi wa mabao 5-0 walioupata dhidi ya Ruvu Shooting mwishoni mwa wiki iliyopita utakuwa unajidanganya, kwani Mbelgiji wao, Patrick Aussems, amesema ndio kwanza shughuli inaanza.

Wekundu hao wa Msimbazi, wamefanikiwa kufunga jumla ya mabao 10 ndani ya siku nne, wakianza kuwaangamiza Alliance mabao 5-1 na baadaye Ruvu Shooting, mabao 5-0.

Walianza kuwabamiza mabao 5-1 Alliance, Alhamisi iliyopita na siku tatu baadaye yaani Jumapili, wakawatoa tena nishai Ruvu Shooting, kwa mabao 5-0, hiyo ikimaanisha kuwa safu yao ya ushambuliaji ina uchu wa kuzifumania nyavu.

Kutokana na ushindi huo mnono katika michezo miwili, baadhi ya mashabiki wanadhani Simba, watabweteka, lakini kocha huyo Mbelgiji amewaambia Jumamosi wasikose kufika Uwanja wa Mkwakwani kushuhudia dozi nyingine ikitolewa.

Simba watakuwa wageni wa JKT Tanzania Jumamosi ya wiki hii katika Uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga, huku kocha wao akitamba kwamba mwendo wao kwa sasa ni wa ushindi tu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.