Baroka ya Abdi Banda inatia huruma Sauzi Afrika

Dimba - - NEWS - NA MWANDISHI WETU

TIMU ya Baroka FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini ‘Absa Premiership’ anayochezea Mtanzania, Abdi Banda, ipo kwenye hali mbaya kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya wanayoyapata.

Baroka inashika nafasi ya 15 kati ya timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo ikicheza michezo 11 na kushinda mchezo mmoja peke yake, ikitoka sare michezo minne huku ikipoteza michezo sita.

Kikosi hicho kitakuwa na kibarua kigumu Jumanne ya wiki inayokuja pale watakapowakabili Orlando Pirates inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 19.

Wapinzani wao hao wamecheza michezo 11 wakishinda mitano, sare michezo minne huku wakipoteza michezo miwili hiyo ikimaanisha kuwa Baroka wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kuondoka na pointi tatu.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.