TENISI WALEMAVU MACHO YOTE CAREN OPEN

Dimba - - NEWS - NA GLORY MLAY

KOCHA wa timu ya tenisi walemavu, Riziki Salum, amesema wanatarajia kuanza kambi mapema kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya Caren Open, inayotarajiwa kufanyika nchini Kenya, Desemba mwaka huu.

Akizungumza na DIMBA, Salum alisema wanatarajia kuanza kambi mapema ili kujipa nafasi ya kufanya ya nguvu na kucheza michezo ya kirafiki ili kujitengenezea mazingira bora ya ushindi.

Riziki alisema wanaendelea na mazoezi japo bado zipo changamoto ambazo wanaendelea kupambana nazo ikiwemo vifaa vya michezo pamoja na viti vya magurudumu.

“Tulikuwa tunafanya tu mazoezi ya kawaida ila tunatarajia kuanza kambi wiki hii ili kujifua zaidi, tutakuwa viwanja vya Gymkhana,” alisema Salum.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.