Ukata waitesa Baobab

Dimba - - NEWS - NA GLORY MLAY

KOCHA mkuu wa timu ya wanawake ya Baobab ya Dodoma, Inocencia Masawe, amesema hali ya ukata iliyopiga kambi ndani ya klabu hiyo imekwamisha ndoto za kusajili nyota wapya.

Akizungumza na DIMBA, Inocencia alisema timu hiyo haina mdhamini yeyote, hivyo zoezi la kupata wachezaji wazoefu kuwa ni ndoto kutokana na mkwamo wa kiuchumi.

Alisema mpaka sasa amebaki na wachezaji chipukizi kwani wakongwe wote wamesajiliwa kwenye timu ambazo zimewatengea mkwanja mnono.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.