Ligi ya magongo kuendelea leo

Dimba - - NEWS - NA GLORY MLAY

TIMU ya mpira wa magongo ya Ukonga itashuka dimbani leo kuwavaa Bomba Mbili, katika mchezo wa Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa shule za msingi na sekondari.

Ligi hiyo imeandaliwa na chama cha mchezo wa magongo Mkoa wa Dar es Salaam (DRHA) katika Uwanja wa JMK Park Kidongo Chekundu ikishirikisha zaidi ya wachezaji 30 wakiwemo wasichana na wavulana wenye miaka 8 hadi 17.

Mbali na mchezo huo kutakuwa na mechi nyingine baina ya wavulana wa Bombambili watakaokutana na Juhudi, huku Amani ikikipiga dhidi ya Kawe A.

Timu ya wavulana ya Bombambili C wao watashuka dimbani kucheza na Ukonga huku Almadrasat itachuana dhidi ya Ukonga B.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), watachuana na wapinzani wao Dar Stars huku Ukonga ikikutana na Amani.

Kwa upande wa wasichana, Nianjema C watashuka dimbani kuumana na Makongo B wakati Kigamboni B wakicheza dhidi ya DI huku wasichana wa Makongo B wakicheza na Twende B.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.