Mrithi wa Aveva, Kaburu kupatikana leo

Dimba - - NEWS -

NA CLARA ALPHONCE KLABU ya Simba leo inatarajia kupata viongozi wapya katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Ocean Road Posta jijini Dar es Salaam.

Wagombea 18 wamepitishwa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba chini ya Mwenyekiti wake, Boniface Lyamwike ambapo leo ndio kila mmoja atajua mbivu na mbichi za hatima yake.

Wagombea 17 wanawania nafasi tano za ujumbe wa bodi huku ile ya Mwenyekiti akigombea Sweddy Mkwabi, pekee baada ya aliyekuwa mpinzani wake, Mtemi Ramadhan, kujitoa kutokana na sababu za kifamilia.

Wajumbe watano wataingia moja kwa moja kwenye bodi ya Wakurugenzi, baada ya Simba kuingia kwenye mfumo wa hisa chini ya mwekezaji, Mohamed Dewji (Mo) aliyeshinda tenda hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Uchaguzi, Stephen Ally, alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na jana walikuwa na kikao cha mwisho cha kamati.

Alisema kabla ya uchaguzi kutakuwa na Mkutano Mkuu na viongozi waliomaliza muda wao watasoma mapato na matumizi kwa wanachama wao kabla ya kukabidhi kijiti cha uongozi mpya ambao utachaguliwa hapo kesho.

Wagombea wanaoingia kwenye uchaguzi leo nafasi ya urais ni Swedy Mkwabi huku wajumbe ni Hussein Mlinga, Iddy Kajuna, Zawadi Kadunda, Mohamed Wandi, Selemani Said, Abdallah Mgomba na Christopher Mwansasu.

Wengine ni Alfred Elia, Ally Suru, Mwina Kaduguda, Said Tully, Jasmine Badar, Juma Pinto, Hamis Mkoma, Abubakari Zebo, Patrick Rweyemamu na Asha Baraka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.