Azam mguu sawa kwa Kagera Sugar

Dimba - - NEWS -

NA EZEKIEL TENDWA KOCHA Mkuu wa Azam FC, Hans van der Pluijm, amesema kikosi chake kipo kamili kuwakabili Kagera Sugar, mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa leo Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam, ambao wanaongoza ligi wakiwa na pointi 27, hawataki kuharibu rekodi yao ya kutokupoteza ndiyo maana wamejizatiti kuhakikisha Kagera Sugar wanakufa kwao.

Pluijm ameliambia DIMBA kuwa anajua ugumu wa michezo ya ugenini lakini atahakikisha wanapambana ili kupata matokeo mazuri.

Wanalambalamba hao wanashika usukani wakiwa na pointi 27 katika michezo 11 waliyocheza wakifuatiwa na Simba nafasi ya pili wakiwa na pointi 26 wakicheza michezo 11 huku Yanga wakishika nafasi ya tatu wakiwa na pointi 25 wao wakicheza michezo tisa.

Michezo mingine itakayochezwa leo, Yanga watakuwa Uwanja wa Taifa kuwakabili Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara, huku Mwadui wakiwa wenyeji wa Tanzania Prisons mchezo utakaochezwa Uwanja wa Mwadui

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.