Juma Abdul hebu msikie kocha wako

Dimba - - NEWS - NA SAADA SALIM

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amehatarisha namba ya beki wake wa kulia, Juma Abdul, baada ya kudai kwamba hata kama atacheza vizuri leo atambue nafasi hiyo ataendelea kucheza kinda Paul Godfery.

Paul alianza kuwika baada ya Juma Abdul kuumia mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar, uliomalizika wa ushindi wa mabao 2-1.

Hata katika mchezo dhidi ya Simba uliomalizika kwa suluhu ya 0-0, alicheza vizuri akikabiliana na akina Emmanuel Okwi na Meddie Kagere kana kwamba ni mchezaji mzoefu.

Juma Abdul atachukuwa nafasi ya kinda huyo anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa katika mchezo uliopita dhidi ya Lipuli FC na kukosa mchezo wa leo dhidi ya Ndanda FC utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na DIMBA, Zahera alisema mechi hii atampa Juma Abdul na hata kama ataonyesha kiwango kizuri kwa upande wake bado ataendelea kumtumia Paul katika mechi zijazo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.