Dareva wasaka wadhamini Uhuru Cup

Dimba - - NEWS - NA GLORY MLAY

KATIBU wa Chama cha Mpira wa Wavu Mkoa wa Dar es Salaam (Dareva), Yusuph Mkarambati, amewataka wadhamini kujitokeza kusapoti michuano ya Uhuru Cup, inayotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Michuano hiyo itashirikisha zaidi ya timu 20 za wanaume na wanawake kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza na DIMBA, Mkarambati, alisema licha ya timu kuanza maandalizi lakini bado wanasaka wafadhili ambao watatoa sapoti katika kuendesha mashindano hayo kwani wao wanasumbuliwa na ukata.

“Bado tunasaka wadhamini, hatuna fedha za kutosha kuendesha mashindano hayo hivyo tunawaomba wadau, makampuni na taasisi kujitokeza ili kuzidi kuukuza mchezo huu hapa nchini,” alisema Mkarambati.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.