AUNTY EZEKIEL

AFANYA KUFURU DUBAI

Dimba - - NEWS - NA JESSCA NANGAWE

MSANII wa Bongo Fleva, Aunty Ezekiel, amesherehekea miaka kadhaa ya siku yake ya kuzaliwa nchini Dubai huku akitumia zaidi ya Sh milioni 10 katika siku yake hiyo.

Akizungumza na DIMBA, Aunty Ezekiel, alisema ameamua kusherehekea siku yake hiyo kama sehemu ya furaha yake akiwa na ndugu zake pamoja na mtoto wake, Cookie huku akidai matumizi ya fedha ni jambo la kawaida kwa siku muhimu kama hiyo.

“Natafuta pesa kwa mwaka mzima, hivyo linapokuja jambo kubwa kama hili sioni tabu kutumia pesa ambayo natafuta kwa jasho, namshukuru Mungu kwa hili na kadiri siku zinavyokwenda nazidi kupata ari ya kutafuta pesa zaidi,” alisema Aunty Ezekiel.

Aunty Ezekiel anadaiwa kutumia kiasi hicho cha fedha, ikiwa sambamba na kufanya manunuzi kwa ajili ya mtoto wake Cookie.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.