Tusubiri kolabo ya Ney na Ali Kiba

Dimba - - NEWS - NA JESSCA NANGAWE

RAPA kutoka kiwanda cha Bongo Fleva, Emanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego, amefunguka na kusema yupo mbioni kuachia ngoma yake mpya ambayo ndani atamshirikisha msanii mwenzake, Ali Kiba. Ney alisema amekua akitamani kuchanganya muziki wake kwa vionjo mbalimbali na safari hii atasikika ndani Ali Kiba. Alisema kuamua kufanya kazi na staa huyo ilikuwa ni moja ya ndoto yake kwani amepanga kuchanganya muziki wake kitofauti ili watu waweze kupata burudani tofauti. “Ni mipango yangu tu, si Ali Kiba wapo wengi lakini nadhani kazi inayokuja atakuwepo yeye, nategemea umoja wetu utazaa kitu kizuri sana ndani yake,” alisema Ney.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.