Choki aibuka na 'Naufunga Moyo'

Dimba - - NEWS - NA JESSCA NANGAWE

GWIJI wa muziki wa dansi nchini 'Kamarade' Ally Choki, amerudi mzigoni kwa kishindo na kuibuka na wimbo mpya 'Naufunga moyo' ambao ni zawadi kwa mashabiki wake.

Choki amerudi kwenye gemu akitokea kitandani ambako alikuwa akiugua maradhi ya kisukari na presha kwa zaidi ya miezi miwili ambapo alilazwa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Akizungumza na DIMBA, Choki baada ya kupita kwenye kipindi kigumu cha kuumwa mahututi sasa afya yake imeimarika na madaktari wamemruhusu kurudi jukwaani.

Alisema wimbo huo umebeba ujumbe mzito kuhusu mtihani wa kuumwa uliompata na tayari ameanza kuufanyia mazoezi na bendi yake ya Super Kamanyola akiwa ameuimba kijana Manjegeka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.