Unakijua kipaji kingine cha Gigy Money?

Dimba - - NEWS - NA JESSCA NANGAWE

STAA wa Bongo Fleva, Gift Stanford maarufu kama Gigy Money, amefunguka na kudai ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuwa mwanasheria na si mwanamuziki kama alivyo sasa. Akizungumza na DIMBA, Gigy, alisema alikua akipenda fani hiyo tangu akiwa mdogo kutokana na kuwa na uwezo wa kumsimamia mtu katika ukweli bila kuyumbishwa. “Nilikuwa napenda sana sheria, sema sikusoma sana na niliishia kidato cha pili lakini ndoto yangu kubwa ilikuwa kuja kuwasimamia watu kupata haki zao, mambo ya muziki nimeyavamia tu,” alisema Gigy Money.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.