BIEBER

MWACHENI TU

Dimba - - NEWS -

HIVI karibuni wakati msaani, Justine Bieber, alipokuwa katika matembezi na mpenzi wake, Hailey Baldwin, alionekana akiwa na mchoro mpya juu ya jicho lake la kushoto karibu na nyusi zake na kuzua maswali mengi kwa waliomfuatilia.

Bieber ambaye aliimba wimbo wa Sorry, amekuwa akijichora michoro mingi katika mwili wake, lakini mpaka sasa hakuna aliyejua maana ya mchoro wake huo mpya uliopo juu ya jicho lake ikiwa tayari ameongeza mwingine kwenye mgongo wake.

Pia, hata mpenzi wake huyo mpya mwenye miaka 21, amejichora kwenye mkono wake wa kulia, alithibitisha hilo mchoraji maarufu nchini Marekani wa michoro hiyo, Keith Mc Curdy.

“Wote wawili wamejichora lakini hawakuniambia nini maana ya michoro hiyo iliyopo mwilini mwao,” alisema Mc Curdy.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.