Cardi B, Nick Minaj wamkosha Chris Brown

Dimba - - NEWS -

HIVI karibuni kumekuwa na ‘bifu’ kali kati ya wasanii wawili wa kike wanaoimba muziki wa hip hop ambao ni Nick Minaj na Cardi B, huku kila mmoja akijiona bora zaidi ya mwingine.

Lakini kwa mujibu wa mtandao wa Hollywood Life, staa wa muziki wa Rnb nchini Marekani, Chris Brown, anadaiwa kufurahia mgogoro kati ya rapa Cardi B na Nicki Minaj.

Chris Brown ambaye mwaka huu amekuwa kando kwenye migogoro, amedai muziki wa hip hop unataka ushindani wa aina hiyo, hivyo haoni tatizo kwa warembo hao kupishana kauli kila siku.

“Chris hana tatizo na Nicki Minaj pia ni shabiki mkubwa wa muziki wa Cardi B, hivyo anapenda kuona wawili hao wakiendelea kuwa na mgogoro ili waweze kuufanya muziki wao kuwa juu zaidi,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.