Eminem aja na ‘sapraizi’ kwa mashabiki wake

Dimba - - NEWS -

MSANII wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Eminem, hivi karibuni aliwashangaza mashabiki wake baada ya kuwaandikia ujumbe kupitia akaunti yake ya Instagram kuwa amenunua tiketi zote za ukumbi wa kuonyesha picha za video.

Huku akiwataka mashabiki wake kuingia bure kuangalia filamu ambayo ameitengeneza kwa kiasi kikubwa ikihusisha maisha yake ya utotoni wakati anaanza muziki iliyotarajiwa kuonyeshwa juzi na jana.

“Nimenunua tiketi zote kwa ajili yenu kuja kuangalia filamu ambayo nimeitengeneza, karibuni wote kuanzia saa 12:40 jioni kujipatia tiketi hizo,” aliandika mwanamuziki huyo aliyetoa albamu yake hivi karibuni ambayo inaitwa Kamikaze.

Hiyo si filamu ya kwanza kufanywa na msanii huyo wa miondoko ya hip hop, alishawahi kutoa moja mwaka 2002 iliyojulikana kwa jina la 8 Mile iliyohusu maisha yake.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.