MAURIZIO SARRI AWAGEUKIA MABEKI

Dimba - - NEWS -

KOCHA wa Chelsea, Maurizio Sarri, amewageukia mabeki wake akiwahitaji waboreshe kiwango chao kwa ajili ya kulinda lango lao vema lengo likiwa ni kutoruhusu mabao mengi zaidi kitu ambacho ni faida kubwa kwa timu.

Chelsea wanaonekana kuwa na mwendelezo mzuri wa ushindani msimu huu chini ya kocha mpya, Sarri, aliyechukua mikoba ya kocha Antonio Conte, majira ya kiangazi.

Kikosi hicho maarufu kama The Blues ambacho jioni ya leo kinatarajia kuvaana na Crystal Palace, hadi sasa hakijapoteza mchezo, kwenye ligi hiyo ambayo ni raundi ya 12.

Sarri aliiambia Sky Sports kuwa: "Najisikia furaha sana kwa aina ya matokeo tuliyovuna, niwapongeze wachezaji kwa kazi kubwa

wanayofanya, lakini tunahitaji kuwa bora zaidi ya hapa.

"Ni kitu kizuri kuonyesha uwezo kila baada ya mchezo, naongelea timu nzima kwa ujumla, lakini idara ya ulinzi inahitaji umakini zaidi, suala ambalo ni la kiufundi zaidi tuna nafasi ya kufanya hivyo,” alisema.

Chelsea ambao watakuwa wenyeji wa mchezo kati ya Palace katika dimba la Stamford Bridge, licha ya kuruhusu mabao saba, wameshinda mechi saba, sare tatu, huku wapinzani wao wakiwa na rekodi mbovu za kushinda mechi mbili pekee kati ya mechi 11.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.