Mwenendo wa nyota na bashira za bahati zinaandaliwa na SHEIKH OMAR BASHO MBEGA (SHUJAH AQRAM). Simu namba 0715 453396 Temeke, Dar es Salaam.

Dimba - - NEWS -

KAA (CANCER) Oktoba 24-Novemba 22

Ukivaa tu pete au ukiweza kutembea na kito chochote cha madini umekuwa umefanya jambo kubwa sana, utafungua milango iliyokuwa imejifunga na hata kama kulikuwa na tatizo kubwa vipi utalitatua kirahisi.

MSHALE (SAGITARIUS) Novemba 23-Desemba 21

Chukua karatasi andika ulichokuwa unakihitaji kwa muda mrefu, kisha ukiweke sehemu unayohifadhia fedha au vitu vya thamani, hakika itakuwa ni sauti yako kwa utakachokiita.

MBUZI (CAPRICON) Desemba 22-Januari 20

Hii ni wiki ya makubaliano kwa lolote utakaloliomba, lakini ni vizuri ukakumbuka ahadi ulizoacha kuzikumbuka kisha ukajaribu kuzifuata tena kinachokukwamisha ni mazingira yako kusahau familia.

NDOO (AQUARIUS) JANUARI 21-FEBRUARI 19

Utafanikisha jambo lililokushinda muda mrefu, lakini utapata msaada huo kutoka kwa rafiki unayemwamini, masuala ya fedha yatakuwa mepesi kwako wiki hii, ila matumizi yatakusumbua.

SAMAKI (PISCES) Februari 20-Machi 20

Maneno mengi yanakufanya ukose uaminifu wa kutosha, unayo nafasi ya kuomba msaada na utasaidiwa, ila epuka hasara usijaribu kufanya biashara usiyokuwa na uhakika nayo.

PUNDA MACHI Machi 21-Aprili 20

Amka asubuhi wiki hii na ufanye maombi ili baraka zako ziwe na uhakika, kumbuka pia sadaka na kufanya ibada itakuongezea nuru ya maisha ya dunia.

NG'OMBE (TAURUS) Aprili 21-Mei 21

Fuatilia ahadi zote ulizoahidiwa huu ni wakati wa kurudisha ulichokitoa, bahati zako zitaendelea kuwa juu, lakini unaweza kuondoa vikwazo kwa kuomba au kupata ushauri.

MAPACHA (GEMINE) Mei 22- Juni 21

Amini kwamba yule umpendaye ana dhamira ya dhati ya kukuacha, hata hivyo anaona aibu kutokana na heshima unayompa. Una nafasi ya kurudisha penzi na heshima kwa kupata msaada wa kinyota.

KAA (CANCER) Juni 22-Julai 23

Kuna mtu anatamani kukudhalilisha ili yeye ajijengee sifa au umaarufu, si kipindi kizuri kupanga miadi na mtu uliyekuwa naye siku nyingi, fanya mambo yako na watu wasiokujua vizuri.

SIMBA (LEO) JULAI 24-AGOSTI 23

Utasikia uonevu aliofanyiwa mtu wa karibu yako nyumbani au kazini, lakini maamuzi yatakusononesha achana nao, hiki ni kipindi cha wewe kufikiria maisha mapya ya kutengwa uliyoanza.

MASHUKE (VIRGO) AGOSTI 24-SEPTEmba 23

Kwa wanaume wana siku tatu nzuri za mahusiano ndani ya wiki hii, pia watapata jambo wanalolihitaji sana kwa ajili ya matumizi ya nyumbani, wanawake watakuwa wenye kusumbuliwa sana wanaume, baadhi yao watakuwa na faida kwao.

MIZANI (LIBRA) Septemba 24-Oktoba 23

Wanaotafuta mchumba, kazi au kuomba kitu fulani watafanikiwa ndiyo wakati mzuri wa kujaribu jambo linalokutia mashaka, hakuna kitakachoshindikana labda kuweza na udhalimu juu yako.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.