HADITHI YA ARSENAL KWA LIVERPOOL INACHEKESHA

Dimba - - NEWS -

ACHANA na mchezo wa usiku wa jana uliowakutanisha Arsenal dhidi ya Liverpool Ligi Kuu, England rejea kumbukumbu za nyuma za wawili hao ni kwamba Majogoo wa Anflied ni balaa. Kabla ya mchezo huo washika mitutu wa London wakiwa uwanja wao wa nyumbani, Emirates ni kwamba walikuwa hawajaonja ladha ya ushindi katika michezo sita ya mwisho ya ligi hiyo. Tangu awali Arsenal ikiwa chini ya Arsene Wenger, kwa muda wa miaka 22, kabla ya kocha wa sasa, Unai Emery, katika michezo hiyo sita waliambulia vichapo mara tatu kama ilivyo upande wa kupoteza. Katika mitanange hiyo, mitano inaonyesha Majogoo wa Merseyside wakiwa chini ya kocha Mjerumani, Jurgen Klopp, huku kinara kwa makocha vikwazo mbele ya Gunners ni Jose Mourinho (12).

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.