AENDE WAPI?

Mojawapo katiya timu hizi itamfaa Ramsey

Dimba - - NEWS -

LONDON, England B AADA ya misimu 11, mechi zaidi ya 300 na medali tatu za ubingwa wa FA, hatimaye ndoa ya muda mrefu ya kiungo Aaron Ramsey na klabu yake ya Arsenal, inaelekea tamati miezi michache ijayo.

Taarifa za Arsenal kutomwongezea mkataba Ramsey ambaye atamaliza muda wa kuitumikia klabu hiyo Juni mwakani, zilitolewa siku chache zilizopita hivyo itakapofika mwishoni mwa msimu huu ataondoka rasmi.

Ramsey amekuwa mchezaji muhimu katika timu hiyo tangu ilipomsajili akiwa kinda, uwezo wake wa kulichezesha dimba la kati ukiwa ndio umemtambulisha kwa muda wote huo.

Ikumbukwe kuwa kiungo huyo aliwahi kupata tatizo kubwa la kuvunjwa mguu na beki wa Stoke City, Ryan Shawcross, lakini alirejea kwa kasi na kuendelea kucheza kwa kiwango cha kuridhisha alipofanikiwa kupona.

Lakini, wakati umewadia kwa Ramsey kutafuta maisha kwingineko na hapa tumekuchambulia timu tatu ambazo zinatajwa kumfukuzia, jinsi gani atakavyozisaidia kulingana na mifumo yao. MAN UNITED

Kiujumla, klabu ya Man Utd ina historia ya kuwanyatia wachezaji Arsenal ambao huwa wanakaribia kumaliza mikataba yao, hivi karibuni walimchukua Alexis Sánchez akiwa amebakiza miezi sita tu ya kuitumikia The Gunners.

Uhamisho huo pia ulimhusisha kiungo mshambuliaji, Henrikh Mkhitaryan, kwenda amekuwa Emirates. na aliyetoka wakati Hata Old hivyo,ánchez mgumu sana Traford na ndani ya United.

Lakini, hilo haliwezikuizuia United isimnyakue Ramsey, kwani bado historia tamu ya mwaka 2012 inaonesha kwamba walipomsajili straika Robin van Persie,bingwa wa Ligi Kuu England kwa maa ya 20 ukatua kwao.

Pia United walimhitajmno kiungo matata, Samir Nasri,ambaye kwa wakati huo aliweka mgmo wa kuongeza mkataba, lakini mshetani wekundu hao walimkos a na kushuhudia akisaini Man City.

Ni wapi sasa ambako Ramsey atachezeshwa katika timu ya United? Bila shaka ni upande wa kuliawa safu ya viungo watatu kwenyemuundo wa 4-3-3 ambao United ya Mourinho imekuwa ikiutumia.

Ramsey atasaidiana na kiungo bora duniani, Paul Pogbahuku Nemanja Mati au Fred wakitumika kama viungo wa dimba la chin

United itafaidika na Ramsey katika suala la ufungaji wa mabao nuwezo wa kucheza pasi fupifupi eneo la hatari pindi watakapokuwa wakicheza dhidi ya timu zinazopaki basi.

Hata hivyo, kuna daliliwamba Ramsey hataiweka kwenyeuwiano sawa safu ya viungo wa Unied kwa sababu kama uwepo wake utmweka huru Pogba, ina maana Mourinho atalazimika kufanya usajili mwingine.

Safari hii, Mourinhotahitaji kiungo mwenye uwezo wa kongeza na kupunguza kasi ya mchezo, atakayeweza kupiga wastani wpasi 70 na zaidi kwa dakika 90, kitu ambacho Ramsey ameshindwa kukonesha tangu msimu wa 2015/16.

Uwezo wa Ramsey ni kupiga wastani wa pasi 49.5 kwa da ika 90. Kwa muda huo, wastani huo nmdogo

zaidi tangu alipoanza kuitumikia Arsenal.

JUVENTUS

Hawa ndio wataalamu wa kusajili wachezaji huru na walio bora duniani kama vile Andre Pirlo, Dani Alves na Emre Can na ripoti zilizopo Italia zinawataja miamba hao wa Turin wanamtaka Ramsey.

Hata hivyo, ni ngumu kuipata nafasi nzuri kwa Ramsey kwenye kikosi cha Juve kama ilivyo rahisi kwa timu za England (kasoro Chelsea), kutokana na kwamba vibibi vizee hao wana viungo mahiri mno.

Chelsea wana viungo mahiri mno hata katika nafasi ya ushambuliaji ambayo Ross Barkley anaitendea haki kwa sasa na bado yupo kinda wao, Ruben LoftusCheek, hivyo nafasi ya Ramsey pale darajani haipo.

Licha ya Juve kupenda wachezaji walio huru, huenda dili hili likaishia kwenye magazeti tu kutokana na kwamba Ramsey hana uwezo wa kumzidi ‘pass master’ Miralem Pjani au Rodrigo Bentancur, wala nidhamu aliyonayo Blaise Matuidi. Viungo hao ndio wanaowafanya washambuliaji wao, Douglas Costa, Federico Bernardeschi, Mario Mandžuki na Cristiano Ronaldo kutesa kutokana na msaada mkubwa wanaowapa katika mashambulizi.

AC MILAN

Vigogo walioanguka barani Ulaya, AC Milan, wapo kwenye mpango wa kujijenga upya na kurudi kwenye zama za dhahabu, inaaminika kama ripoti zinavyodai kuwa wanamfukuzia Ramsey kwani wanaona ni mchezaji atakayewafaa.

Rossoneri hao wana viungo wazuri lakini hawana ubora kama walionao wale wa Juventus. Nyota kama Giacomo Bonaventura, Lucas Biglia na Franck Kessié wote ni wachezaji wazuri, lakini uwepo wa Ramsey utaongeza nguvu zaidi.

Iwapo kikosi hicho cha kocha, Gennaro Gattuso, kitafanikiwa kumaliza katika nafasi ya nne au zaidi kwenye msimamo wa Serie A, watarudi Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, hivyo Ramsey akiamua kujiunga nao, itakuwa poa zaidi.

Ramsey atasaidiana na kiungo bora duniani, Paul Pogba, huku Nemanja Mati au Fred wakitumika kama viungo wa dimba la chini.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.