ROMARII - 31

Onesho la Washirika lavunja rekodi ya viingilio

Dimba - - NEWS - Itaendelea ....

ILIPOISHIA TOLEO LILILOPITA Kulikuwa na tafsiri mbalimbali kuhusiana na wimbo huu: 'Yaliyopita si ndwele', kwamba 'Komandoo' alitunga akiulenga uongozi wa Vijana Jazz, ambao wakati ule ulikuwa chini ya Hemed Maneti, aliyefahamika kwa jina la kimuziki 'Chiriku'. #####

Hapa Romarii anakiri ukweli kuwa, nyimbo nyingi za wanamuziki wa zamani zilitungwa kutokana na matukio yaliyowagusa wanamuziki binafsi ama mikasa ya ndani ya jamii.

Kwa mujibu wa maelezo ya Eddy Sheggy, aliuelezea wimbo huo 'Nimekusamehe Lakini Sitokusahauí, ulikuwa ni kisa ambacho Hamza Kalala alipopata ajali ya gari na alipopewa mapumziko ya kujiuguza ndipo Vijana Jazz ilipotafuta mpiga gitaa la solo mwingine.

Simulizi hii ilibainisha kuwa, wakati 'Komandoo' Kalala anauguza majeraha ya ajali hiyo, ndipo kukasikika taarifa za kwamba Vijana Jazz walimleta kundini mpiga solo kutoka bendi ya Tancut Almasi ya Iringa.

Huyu alikuwa Shabani Yohana ë Wantedí, ambaye wakati huo alipojiunga na Vijana, alikuwa bado kijana mdogo.

Pamoja na ukweli kuwa haikuwahi kuthibitishwa juu ya ukweli huo, lakini wapembuzi wa masuala ya muziki walilinasibisha tukio hilo na utunzi wa kibao hicho cha 'Nimekusamehe, lakini sitakusahau'.

Ikaonekana kama 'Komandoo' aliutumia wimbo huo kama 'dongo' la salamu kwa uongozi na hasa Hemed Maneti ambaye ndiye mtu wa mwisho kuidhinisha ajira ya mwanamuziki ndani ya Vijana Jazz.

Kwa mujibu wa mazungumzo yangu na Eddy Sheggy ya wakati ule wa uhai wake ni kwamba, baada ya tukio hilo la kuletwa kwa Shabani Yohana ë Wantedí, ndilo lililochangia 'Komandoo' Kalala kuachana na Vijana Jazz.

Ilitajwa kuwa ndiyo sababu ya 'komandoo' kuanza kwa vuguvugu la kuanzishwa kwa bendi ya Washirika Tanzania Stars.

Hata hivyo, Sheggy alisimulia namna wanamuziki wengi waliotoka Vijana Jazz na kujiunga na Washirika walivyokuwa na hamasa kubwa ya kutaka kutunga na kupiga muziki katika kiwango cha kutaka kusambaratisha 'ngome' ya upande wa kule walikotoka.

Katika mkakati huo, ndipo kila mwanamuziki alijikuta akitunga na kuimba nyimbo ambazo kwa wakati ule ziliwavutia mashabiki nchi nzima.

Hili lilifanikiwa katika maonesho yao ambayo yaliweza kuhudhuriwa na mashabiki wengi ndani na nje ya jiji la Dar es Salaam.

Iliezwa kuwa, katika moja ya onesho lililofanyika nje ya jiji la Dar es Salaam, ndilo lililodhihirisha namna Washirika walivyokuwa na washabiki wengi.

Katika onesho moja lililofanyika mkoani Dodoma, bendi hiyo iliweza kuvunja rekodi ya kupata fedha za kutosha, hasa kupitia viingilio.

Onesho hilo lilifanyika katika ukumbi wa Dodoma Hotel, ambako kwa mujibu wa simulizi ni kwamba, Washirika Stars iliingiza jumla ya Sh 17,000. Hii ilikuwa mnamo mwaka 1989.

Ilielezwa kuwa, wakati huo kiasi cha fedha kilikuwa kikubwa kuwahi kulipiwa kilichohusisha mapato ya bendi kupitia viingilio vya mlangoni.

Simulizi zinasema kuwa, onesho hilo lilikuwa mahususi kwa ajili ya kuwaburudisha waheshimiwa wabunge ambao walikuwa mjini Dodoma kwa ajili ya vikao vya Bunge la Jamhuri vya mwaka ule.

Ni onesho lililotajwa kuwa lilivunja rekodi kwa bendi ya muziki kupata kiasi hicho cha fedha kupitia tumbuizo moja tu la ukumbini. Hapo ndipo Washirika Stars chini ya 'komandoo' Hamza Kalala ilipoonekana kuwa bendi iliyoweza kupata washabiki wengi katika kipindi kifupi tu tangu kuanzishwa kwake.

Hili liliungwa mkono na Romarii, ambaye alipojiunga na Washirika Stars mwaka 1981, aliikuta bendi ikiwa na wanamuziki waliojipambanua kuwa na mkakati wa kuifanya bendi kupiga muziki wa kisasa unaowavutia wengi.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.