MANARA SAFARI HII KAMVAA MAUA SAMA

Dimba - - NEWS -

MSEMAJI wa Simba, Haji Manara, kila wakati amekuwa ni mtu wa kutoishiwa maneno na safari hii kapisha hodi kwa staa wa muziki wa kizazi kipya na kumpa ujumbe huu.

Kupitia ukurasa wake, Manara ameandika: Maua Sama ni mrembo kweli kweli na ana kipaji maridhawa cha kuimba, kisha ana heshima ya hali ya juu na kwa kuwa akili yake si ya kuvukia mwendokasi, naye ni shabiki wa Simba.

TSHABALALA ASHEREHEKEA ‘BIRTHDAY’ YAKE HIVI

BEKI wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, mwishoni mwa juma alisherehekea siku yake ya kuzaliwa huku mastaa mbalimbali wakimpongeza kwa hatua hiyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Tshabalala aliamua kuposti kipande cha video kikimwonyesha akiwa na wachezaji wenzake ambao walikuwa wakimpongeza kwa kummwagia maji na kumpaka keki mwili mzima huku wakimwimbia…kitendo hicho alikifurahia na kuandika hii ndio maana halisi ya neno SIMBA… NGUVU MOJA.

PASCAL WAWA ANAVYOFANANISHWA NA VIDAL

KUNA msemo wa Kiswahili ambao umezoeleka sana unaosema, Duniani wawili wawili, basi hivyo ndivyo wachezaji hawa wawili beki wa Simba, Pascal Wawa na kiungo wa FC Barcelona, Arturo Vidal, ambao huenda hata hawafahamiani lakini picha zao zinaangaziwa zaidi kuwa ni watu ambao wanafanana kwa mwonekano wao.

Katika mwonekano wa kawaida, Wawa na Vidal wanafanana katika mtindo wao wa nywele ambapo wote wamenyoa pembeni na kubakiza kidogo katikati ya kichwa ambazo zinaelekea kichogoni.

WEMA SEPETU MAHAKAMANI TENA

MSANII wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu, Novemba 01, 2018, ameachiwa kwa dhamana katika Mahakama ya Kisutu, jijini Dar es Salaam kwa kosa la kusambaza picha za faragha mtandaoni.

Wema Sepetu alipata dhamana mahakamani hapo baada ya kukidhi vigezo, ambapo moja ya sharti lilikuwa ni kupata mdhamini mmoja atakayesaini bondi ya Sh milioni 10 sambamba na sharti jingine alilopewa kwenye dhamana hiyo, ni kutoposti picha au video zenye maudhui ya ngono kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

IDRIS AMWAGA AJIRA KWA VIJANA

MCHEKESHAJI Idris Sultan, ameamua kutoa fursa kwa vijana wa Kitanzania na kuahidi kuwapa vijana 15 ajira, hii ni baada ya kufikisha wafuasi milioni 3 kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kupitia ukurasa wa Instagram… “Nimefikisha followers milioni tatu na kushukuru jamii kwa hilo, nitawapa ajira vijana 15, vijana watano kwa kila milioni. Pata kwa jamii rudisha kwa jamii.

MCHEKI WIZKID, AFANYA KUFURU KWENYE LAMBORGHIN

STAA wa muziki nchini Nigeria, Wizkid, ameripotiwa kununua gari la kifahari aina ya Lamborghin lenye thamani ya Naira milioni 101 ambazo ni sawa na zaidi ya milioni 700 za Bongo.

Wizkid aliamua kupost sehemu ya video kwenye ukurasa wake ukionyesha aina hiyo ya gari huku mashabiki zaidi ya milioni mbili ndani ya saa 48 wakiitazama.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.