Pochettino: Sina ushawishi zaidi ya klabu

"Najua ni kwa ajili ya klabu ambayo ndiyo sababu yetu sote kuwepo hapa kwa huduma zao na ilivyowekeza kwa mambo...

Dimba - - NEWS -

KOCHA wa Tottenham, Mauricio Pochettino, haamini kama ana ushawishi mkubwa wa kumfanya mchezaji asaini kwa ajili yake kuliko nguvu ya klabu tofauti na inavyoelezwa.

Hivi karibuni kiungo Mwingereza, Dele Alli, alisaini mkataba wa muda mrefu wa miaka sita kuendelea kusalia mahali hapo hadi 2014 akiungana na kina, Harry Kane, Erik Lamela, Heungmin Son, Davinson Sanchez na Harry Winks.

Alli baada ya kusaini mkataba huo alimmwagia sifa kocha, Pochettino, ingawa Muargentina huyo ambaye amekuwa miongoni mwa makocha lulu barani Ulaya, anaamini klabu ina nguvu sana.

"Najua ni kwa ajili ya klabu ambayo ndiyo sababu yetu sote kuwepo hapa kwa huduma zao na ilivyowekeza kwa mambo, naamini Delle au mchezaji mwingine yeyote atasaini mkataba kwa ajili ya klabu na si mimi.

“Kwa ajili yangu eti iwe hivyo, si sahihi, binafsi nawajali sana wachezaji wangu, narudia majukumu yangu nayajua, inatakiwa tuwe makini na usajili wa Januari,” anasema Pochettino.

POCHETTINO

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.