RC Gambo adaiwa kutuma polisi kuzuia rambirambi

Wavamia shule ya watoto waliopata ajali, Meya waandishi wakamatwa

Mtanzania - - Mbele - Na WAANDISHI WETU -ARUSHA

JESHI la Polisi mkoani Arusha limewakamata viongozi wa Shirikisho la Wenye Shule na Vyuo Binafsi nchini waliokuwa wamekwenda kutoa rambirambi kwa wazazi na walezi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Lucky Vincent waliofariki dunia kwa ajali ya basi hivi karibuni.

Wengine waliokamatwa ni Meya wa Jiji la Arusha, Kalisti Lazaro ,waandishi wa habari 10 kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliokuwa wakifuatilia tukio hilo,viongozi wa dini wanne, Mkuu wa Shule na Diwani wa Kata ya Olasiti.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Yusufu Ilembo, alithibitisha kuwa amri ya kuwakamata viongozi na waandishi wa habari wakati wakitekeleza majukumu yao, ni agizo la Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.