Mtoto wa Ndama akiri kutakatisha fedha

Mtanzania - - Mbele - Na KULWA MZEE -DAR ES SALAAM

MFANYABIASHARA maarufu nchini Ndama Shabani Hussein ‘Pedeshee Ndama mtoto wa Ng’ombe’, amekiri kutakatisha Dola za Marekani 540,000.

Ndama amekuwa mshtakiwa wa kwanza kukiri katika makosa ya utakatishaji fedha haramu ambapo adhabu yake kisheria ni kulipa faini si chini ya Sh milioni 100 na isizidi Sh milioni 500 au kwenda jela miaka isiyozidi 10 na isiyopungua miaka mitano.

Mshtakiwa huyo alikiri kosa hilo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Mwandamizi, Victoria Nongwa. Akiiwakilisha Jamhuri, Wakili

wa Serikali, Esterzia Wilson alidai mshtakiwa huyo alikiri Mei 16, mwaka huu na alitakiwa kusomewa maelezo ya awali dhidi ya shtaka hilo la kutakatisha fedha.

Alidai Ndama alikiri kosa moja la sita na kuyakana makosa mengine matano yakiwemo ya kughushi.

Esterzia alidai mshtakiwa alipaswa kusomewa maelezo ya awali lakini haikuwezekana kwa sababu jalada la kesi hiyo lililopo Polisi halijafika kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Hakimu Nongwa alikubaliana kuahirisha kesi hiyo hadi Mei 24, mwaka huu kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali kwa shtaka la sita na mashtaka mengine matano upelelezi wake haujakamilika.

Mei 16, mwaka huu, Ndama alikubali kosa la sita la kutakatisha fedha baada ya kusomewa mashtaka upya kutokana na upande wa Jamhuri kufanyia marekebisho hati kama walivyokuwa wameamriwa na mahakama.

Katika shtaka la sita, ambalo Ndama amekubali kati ya Februari 26 na Machi, 2014, Dar es Salaam, akiwa mwenyekiti na mtia saini wa Kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Limited na akaunti ya benki ya kampuni hiyo iliyoko katika Benki ya Stanbic alijihusisha moja kwa moja kwenye uhamishaji fedha Dola za Marekani 540,000 na kuzitoa huku akijua au alipaswa kujua fedha hizo ni zao la kosa la uhalifu la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

OSCAR ASSENGA IKULU MIAMBA: Mpasuaji wa miamba kutoka Kampuni ya Makudo ya Mkoani Kilimanjaro, akipasua miamba iliyoziba barabara ya Mombo- Lushoto mkoani Tanga jana kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha hivi karibuni.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.