Wanaotoa matusi hadharani kuchapwa viboko

Mtanzania - - Mbele - Na UPENDO MOSHA - MOSHI

WANANCHI wa Kijiji cha Kyou Kata ya Kilema Kaskazini halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro wamekusudia kutunga sheria ndogo zenye lengo la kuwabana watu wanaotoa lugha za matusi hadharani.

Hayo yalielezwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Hipolity Lyimo alipozungumza katika mkutano mkuu wa halmashauri ya kijiji.

Alisema hatua hiyo imefikiwa kutokana na kukithiri lugha chafu za matusi kijijini hapo.

Alisema sheria hizo ndogo zitakuwa adhabu tofauti tofauti ambazo mbali na faini, pia mtuhumiwa atakayebainika kutenda kosa hilo atachapwa viboko hadharani kusaidia kudhibiti mmomonyoko wa maadili katika jamii na kurejesha nidhamu ambayo kwa sasa imeonekana kushuka.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.