Katavi, Songwe na Rukwa kuunganishwa na Daraja la Momba

Mtanzania - - Mkoa - Na RAMADHAN HASSAN

UJENZI wa Daraja la Momba unatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha wa 2017/2018, huku Sh milioni 2,935 zikitengwa kwa ajili ya ujenzi.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani, alitoa kauli hiyo bungeni jana, wakati akijibu swali la Mbunge wa Momba (Chadema), David Silinde.

Ngonyani alisema Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), yupo katika hatua za mwisho kumpata mkandarasi kwa ajili ya kuanza ujenzi.

Alisema licha ya serikali kutenga Sh milioni 2,935, pia imetenga Sh milioni 3,000 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi huo katika mwaka wa fedha 2017/2018.

Naibu Waziri huyo alisema barabara hiyo ni kiungo muhimu katika barabara ya Kibaoni hadi Kansansa kwenda Muze hadi Ilemba na Kilyamatundu hadi Kisamba na Mlowo, ambayo inaunganisha mikoa ya Katavi, Rukwa na Songwe.

Pia, alisema barabara hiyo ni kiungo muhimu, kwani inapita katika Bonde la Ziwa Rukwa ambalo ni maarufu sana kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.