MALALAMIKO YA BONGO MUVI YANA UKWELI LAKINI WAMEKOSEA

MUHOGO MCHUNGU, JIMMY CLIFF & RAY KIGOSI:

Mtanzania - - Swaggaz -

H AMKANI si shwari kwa waigizaji wetu kutoa povu zito walipotishia kuingia barabarani kupinga tija finyu, kutokana na kulundikana muvi za nje kwa bei chee zinazosababisha kufifia kwa soko lao ilihali wanafanya kazi kubwa kutengeneza filamu zao. Nimekupangia majina hapo juu yaliyotamba katika zama tofauti ili kujenga muktadha wa kudadavua suala hilo kwani tukisaidiana weledi jinsi mambo yalivyokuwa, utawaelewa Bongo Muvi ingawa staili yao ya kuwasilisha kinachowakera ndiyo ilikosewa lakini wanacholalamika kina ukweli mwingi kuliko inavyodhaniwa na wengi kuwa hawana jipya, wanatapia ustaa unaofifia. Nakita kisu kwenye mfupa nikikufafanulia ‘Back’ ilivyokuwa kabla sijakutupa ‘Front’ ilivyo sasa na kuweka sawa palipokosewa na kupatiwa. Muhogo Mchungu ninayemzungumzia ni Hayati Mzee Rashid Kawawa a.k.a Simba wa vita anayefahamika zaidi katika harakati za kisiasa, lakini ndiye Mbongo wa akitumia jina hilo la Muhogo katika muvi inayoonesha kijana aliyetinga mjini kusaka maisha yaliyomshinda akaanza kupiga finga.

Ni muvi ya kitambo sana (Back) sisi wenye makamu yetu tulibahatika kuiona kabla haijasundwa kutokana na nafasi yake serikali, zamani hizo za muvi za black & white kwenye majumba ya sinema kabla muvi haijaanza lazima msimame wimbo wa Taifa unapopigwa, uzalendo uligubika! Jimmy Cliff ni mwanamuziki wa Reggae wa Jamaica lakini umaarufu uliomwezesha kutoboa ulitokana na kuigiza muvi ya ‘The Harder They Come’ iliyobeba ‘Soundtracks’ za nyimbo zake, simulizi yake inafanana na muvi ya Mzee Kawawa sina uhakika kama walikopiana na ‘ku-paste’ lakini ilikuwa muvi bomba.

Ray Kigosi hana haja ya kumtambulisha anafahamika kwamba ni miongoni mwa waigizaji nguli wa sasa wa kiume hapa Bongo. Nakutupa ‘Back’ ya Mzee Kawawa kwani licha ya kuigiza alikuwa mwongozaji msaidizi, mweledi wa kuandaa muswada (script) na nafasi nyingine nyingi kwenye filamu alizoshiriki.

Tujikite ‘Front’ kwa Jimmy Cliff kwamba maudhui yalitengenezwa kumkubalisha kupitia muvi ingawa alikuwa mwanamuziki, akafanikisha mauzo makubwa ya nyimbo zake kwa hiyo lengo lake lilitimia. Bongo Muvi ya akina Ray na wengine licha ya upungufu kwenye matoleo yao tukubali kuwa kama ilivyofanya Bongo Fleva kukatiza mikong’osio ya nchi jirani kutugubika tukageuzia masikio mikong’osio ya hapa, hata Bongo Muvi imefanya hilo lakini tasnia hiyo inakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwemo udumavu wa ubunifu na stori za muvi zilizotoholewa kwenye muvi za nje za zamani, tuliokuwepo tangu kitambo hicho tunazifahamu.

Pia kuna tatizo kwenye uhusika (casting), umakini wa uhariri na mpangilio wa uchukua matukio (cinematography), hata kuchanganya lugha kwa lafudhi tenge za Kiingereza ikiwemo tafsiri ya Kiingereza (Sub-titles) zilizokosewa kwa kutofahamu vyema lugha hiyo.

Lakini jiulize, kwa gharama za uzalishaji zisizolingana na kinachorudi kwenye mauzo hata ungekuwa wewe ungezingatia sana wekedi badala ya ‘kata funua’ ili ulambe chako maisha yaende? Kwa lundo la muvi za kigeni zinazoingia nchini zilizorudufiwa kinyume na sheria zinazouzwa kama mafungu ya karanga mtaani kwa bei rahisi, ungenunua muvi moja kwa shilingi elfu tatu badala ya hamsini kwa bei hiyo? Kama zinaingizwa kihalali zilipe kodi halali ili kuweka ushindani wa soko na za Kibongo, ingekuwa hivyo uwekezaji makini ungekuwepo.

‘Front’ wanayopaswa kuja nayo Bongo Muvi siyo kuandamana watumie vyama vyao halali kubainisha takwimu na kodi ambayo serikali inaikosa, kwa kulinganisha na Mashariki ya kati tunakoshobokea tamthilia zao bila kujua serikali zao ziliwakingia kifua.

Kwamba ukiwa na demu atakwambia nakukubali ulivyo kwa kila kitu ila usikubali. Tafuta kila kitu ambacho huna kisha kimiliki bila kumuuliza.

Kwa sababu

kwanza kuigiza muvi

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.