Maduu dizaini kama mnazingua hivi

Mtanzania - - Swaggaz - Na RAMADHANI MASENGA

U KIWA na hela halafu ‘hupigi kazi ya maana katika uwanja wa fundi seremala’, demu atakwambia hela hata kwao wanazo. Hivyo atakusanua kuwa kheri aondoke kuliko kukaa na wewe.

Ukiwa na hela na kazi unapiga, demu anaweza kuwaambia mashosti zake kuwa huna mvuto hivyo hajisikii raha kuongozana na wewe.

Ukiwa bishoo kinoma, kila nguo ikitoka unayo, vipuri kibao kama Nelly, demu anaweza kumwambia dada yake kuwa wewe siyo mwanume kamili. Kwamba anataka mwanaume mwenye tabia za kigumu ili hata akiwa naye ajue yuko na mwanume halisi.

Kuna baadhi ya mademu nuksi aisee. Kila ulicho nacho wao hawakitaki ila kila ambacho huna wao ndiyo wanakililia. Sizingui masela. Anza kuangalia kuanzia leo.

Kuwa bize na kazi, tafuta mtonyo, nunua majumba na magari kibao. Anzisha biashara kila leo. Utakuja kusikia demu akimlalamikia dada yake kwamba uko bize sana na kazi hata unamsahau yeye.

Kwamba haoni thamani ya kuishi na wewe kwa sababu unamfanya ajihisi kama mlinzi wa nyumba. Wapeni hongera mademu aisee.

Hawaeleweki halafu dizaini kama hawajui wanachokitaka, jaribu kubalansi maisha uone. Kazi kidogo na mapenzi kwa sana. Kitakachotokea utabaki kinywa wazi.

Kwa kuwa unabalansi basi unaweza kumudu kujenga amani katika nyumba yako kisha ukanunua Carina yako mpya kutoka Japan kwa ajili ya misele na mitoko ya familia.

Sasa usiombe uko na demu wako kisha kidume kingine kiwapite kiwe ndani ya Prado New Model. Demu anaweza kuropoka: “Wanaume walee na magari ya maana wanapita, siyo sisi tuliominyama katika mkokoteni.”

Yaani wewe mwenye Carina dizani kama siyo mwanamume wa nguvu. Mademu mnataka nini kwani? Pale unapodhani wanataka brotherman, unakuja kugundua wanataka kibosile wa ofisini.

Ukijidanganya kuendelea kuamini hivyo baadaye unagundua akikaa na mashosti zake anaponda vibosile. Kwamba wamekaa kizee, eti hawavutii kwa sababu wanaishi kiboya boya.

Zamani niliamini uchawi wa mademu ni hela. Basi kila nilipoomuona mtu ana hela nilijua kayaweza mahusiano yake. Kumbe nilikuwa najiongopea kichizi.

Kuna mwana mmoja alikuwa ana pesa mingi sana. Basi kila nikimwona akipita na chombo yake, ambaye ni mkali kinoma, nilijua mchizi kaweza sana katika maisha ya kimapenzi. Kumbe dah majanga matupu.

Nilipopata habari za yule demu nilichoka kinoma. Kumbe pamoja na mihela yote anayopewa, miwikiendi yote wanayotoka pamoja na kupewa uhuru na mchizi wa kutumia magari na mali zake kinoma.

Demu alikuwa akimsaliti mchizi kwa boya mmoja, mtoto wa mama asiye na kazi wala kibarua. Mbaya zaidi demu yule alikuwa akitumia ndinga ya mwana kutanua na kale katoto ka mama katika mitaa na mahoteli ya jiji kipindi ambacho mwana yuko kazini akiminyama.

Mademu mnataka nini? Pesa, mabrotherman, wapiga kazi ama walamba midomo maskani? Hamueleweki aisee!

Mwanangu mmoja baada ya kusalitiwa na chombo yake aliwahi kusema mademu hawahitaji chochote ila wanahitaji chochote.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.