Soya inahitaji mazingira haya

Mtanzania - - Jiongeze -

SWALI: Jina langu ni Samsoni Nkonda naishi Mtwara, je zao la soya za lishe linahitaji mazingira gani, maana nimesikia lina faida nyingi.

JIBU: Nkonda kilimo cha soya (soya beans) kinahitaji mvua ya kutosha ya wastani wa milimita 350 hadi 1,500 kwa mwaka inayonyesha katika mtawanyiko mzuri au kufanya kilimo cha umwagiliaji.

Hii ni kuhakikisha upatikanaji wa unyevu wa kutosha kuanzia upandaji hadi inapotoa maua na matunda. Pia huhitaji udongo wenye rutuba na usiotuamisha maji, hivyo kama shamba halina rutuba ya kutosha, ni muhimu kutumia mbolea.

Ni muhimu kuzingatia misimu ya mvua ya mahali husika na aina ya soya inayofaa ili kuruhusu soya kukomaa wakati hakuna mvua na hivyo kuhifadhi ubora wake Mikoa inayoongoza kwa uzalishaji ni pamoja na Ruvuma, Mbeya, Rukwa, Iringa na Morogoro lakini pia mikoa ya Tanga, Lindi, Kagera, Mara, Kigoma, Kilimanjaro, Arusha na Manyara inafaa kwa kilimo hiki.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.