Mambo manne kuzigatia kutambua mbegu bora

Mtanzania - - Jiongeze -

KATIKA safu ya pata maujuzi leo tunakuletea mambo ya kuzingatia kutambua mbegu bora.

Mbegu bora zitazalisha mazao bora yatakayofaa soko na kukuingizia kipato.

Mambo muhimu manne ya kutambua ubora wa mbegu

KWANZA KUJUA ASILI YA MBEGU

Mbegu ambazo zipo sokoni ni zile ambazo aidha zimechavushwa kwa njia ya asili (OPVs) au chotara (F1).

Mbegu zilizochavushwa kiasili huzalishwa

katika mazingira ambayo uchavushaji hausimamiwi, na matokeo yake ni mbegu huwa na tabia zinazotofautiana.

Mbegu chotara huzalishwa katika mazingira yanayosimamiwa kwa uangalifu .

Ushavushwaji hufanywa kati ya wazazi tofauti kwa lengo maalumu ya kupata tabia bora, ambazo zinatakwa na mkulima.

Kwa vile uzalishaji unasimamiwa kwa uangalifu, kiwango cha ubora kiko juu kuliko mbegu zinazochavushwa kiasili.

PILI CHANZO CHA MBEGU,

Kwa kawaida chanzo huhakiki ubora wa mbegu. Daima chagua mbegu kutoka vyanzo vinavyo aminika. Vyanzo vinavyo aminika, kama kampuni zinazo zalisha mbegu, hutoa taarifa zaidi juu ya mbegu na pia hutoa msaada kwa wakulima pale wanapohitaji. Pia, pata mbegu kutoka kwa wauza pembejeo wasiokuwa na historia ya kuuza bidhaa feki.

Tatu Maagizo/maelezo maalumu (specifications)

Mbegu bora hufafanuliwa kwa mbegu yenyewe na muundo maalumu wa ufungashaji wake.

MAAGIZO

maalumu hujumuisha taarifa za uotaji na nguvu ya mmea, asilimia ya ubora na kinga dhidi ya magonjwa.

Maagizo ya ufungashaji huhakiki ubora na huweka kumbukumbu. Hivyo hujumuisha jina la kampuni ya

uzalishaji (chanzo), jina la aina ya mbegu, nambari ya mfungasho (batch number) na tarehe ya uzalishaji.

Hatua za kuchagua mbegu bora

Kujua jina la aina ya mbegu husaidia katika uchaguzi wa mbegu maana ita athiri maagizo maalum ya mbegu.

Ni muhimi mkulima kuiangalia mbegu uhimili wa magonjwa na wadudu, Majira ya kusia na kupanda Mazingira Maji, joto, udongo.

NNE HALI YA UHIFADHI.

Mbegu zinatakiwa zihifadhiwe katika mahali penye ubaridi lakini pakavu ilikulinda

UBORA. 1

Katika mipango ya kulima mboga mboga, wakulima hufanya maamuzi ya mboga watakazo lima kuendana

na mahitaji sokoni hivyo huchagua mbegu bora kwa kuwa zina faida.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.