IRENE

Mwanangu ndiyo kila kitu

Mtanzania - - Swaggaz - Na KYALAA SEHEYE

MREMBO anayefanya vyema kwenye tasnia ya filamu nchini, Irene Uwoya amefunguka kuwa mtoto wake, Krish aliyezaa na mcheza soko Ndikumana Kataut ni kila kitu kwake na anapomkosa

kwa muda mfupi huwa anaishiwa nguvu.

Uwoya ameliambia Swaggaz kuwa hata kama mtoto wake amelala chumbani kwake huwa anakwenda kumwangalia ili moyo wake uweze kutulia.

“Hii hali sijui inakuwaje yaani naamini damu nzito kuliko maji, nafahamu kuwa mwanangu anapata kila kitu kinachotakiwa ila nisipomuona naishiwa nguvu, nikiwa nje ya nchi nalazimika kuongea naye ili nisikie sauti yake na kupata nguvu,” alisema Irene Uwoya.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.