PAM D arudi nyumbani kwao kwa kishindo

Mtanzania - - Swaggaz - Na MWANDISHI WETU

MIEZI kadhaa baada ya kumpoteza baba yake ambaye alizikwa nyanda za Juu Kusini, nyota wa Bongo Fleva Pamela Daffa ‘Pam D’ amelazimika kuwashukuru mashabiki zake kwa kufanya onyesho maeneo ya Mafinga mkoani Iringa.

Pam D, ameliambia Swaggaz kuwa ni mara yake ya kwanza toka apate msiba kutua mjini humo hivyo onyesho hilo litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Africabanna litakuwa ni fursa kwake ya kukutana na mashabiki wa eneo hilo. “Iringa ni nyumbani, kesho (leo) nitakuwa Mafinga kwa hiyo mashabiki zangu waje, tupeane burudani na nitagonga ngoma zangu zote kali,” alisema Pam D.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.