Nikki wa Pili awakingia kifua mabinti

Mtanzania - - Swaggaz - Na JOHANES RESPICHIUS

STAA wa muziki wa Hip Hop nchini, Nickson Saimon ‘Nikki wa Pili’ amewakingia kifua wanafunzi wa kike wanaopewa ujauzito wakiwa shuleni kuwa hatua ya kuwafukuza shule ni kuwatengenezea mazingira mabaya watoto watakaozaliwa.

Staa huyo wa singo ya Sweet Mangi, alitumia ukurasa wake wa Instagram kuchangia mjadala huo uliolitikisa Bunge wiki hii na kudai kuwa kumfukuza na kumzuia kurudi tena shule ni kumtengenezea mazingira ya uchokoraa mtoto atakayezaliwa.

“Kumfukuza msichana mjamzito shule ni sawa na kumfukuzia mtoto atakayezaliwa kwenye uchokoraa hivyo kuangamiza kizazi kilichopo na kijacho,” alisema Nikki.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.