bado yupoyupo sana

Mtanzania - - Swaggaz - LAGOS, NIGERIA

NYOTA wa muziki nchini Nigeria ambaye anatamba na kibao chake Come Closer, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’ amefunguka mara baada ya kupata mtoto wake wa pili kuwa hana mpango wa kuoa siku za hivi karibuni.

Msanii huyo wiki iliyopita aliweka wazi kuwa amepata mtoto wa pili wa kiume akiwa na mpenzi wake Binta Diamond, hivyo mashabiki wake wengi kupitia mitandao ya kujamii walikuwa akijiuliza kama anatarajia kufunga ndoa na mrembo huyo siku za hivi karibuni.

“Furaha yangu kubwa kwa sasa ni kwamba nimepata mtoto mwingine wa kiume, hivyo nitakuwa na watoto wawili na familia yangu inakuwa kubwa.

“Kuwa na watoto haina maana kuwa unatarajia kufunga ndoa na mama wa watoto hao, ukweli ni kwamba mipango yangu ya ndoa bado kabisa na wala sina ratiba hiyo kwa sasa,” alisema Wizkid.

Newspapers in Swahili

Newspapers from Tanzania

© PressReader. All rights reserved.